Azam FC tayari imefanya nyongeza ya wachezaji takribani watano katika kikosi chao, ukijaribu kutazama kile walichokuwa wanakifanya katika klabu zao za awali wengi wao walikuwa wanafanya vizuri.

Bila shaka matarajio ya viongozi wa Azam ni kuona wachezaji hawa wanakuwa katika viwango bora na kuisaidia timu, wana deni kubwa mbele yao ambalo wanapaswa kulilipa.

Jukumu ninaloliona mbele ya George Lwandamina ni kuona ni namna gani anaweza kuwaunganisha wachezaji hawa ndani ya muda mfupi.

Tayari wameshasajili nusu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza hii ina maana timu itakuwa na sura nyingi ambazo ni mpya.

Kitu kizuri ni wachezaji takribani wote waliosajiliwa mpaka sasa wanatoka katika ukanda mmoja hivyo basi pengine George Lwandamina asiwe na kibarua kikubwa sana kuwaunganisha.

Kila la kheri kwake.
Imeandikwa na swalehmawele

Arteta: Namuhitaji Xhaka
Kabwili aomba radhi, akiri kufanya kosa