Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amethibitisha kifo cha mshindi wa Nobel na miongoni mwa watu muhimu kumaliza ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Askofu Emeritus Desmond Tutu

Desmond Tutu amefariki katika umri wa miaka 90 kwa sababu za kiafya ambazo ni kusumbiliwa na Saratani ya Kibofu

Tutu aligundulika kuwa na saratani ya kibofu mwishoni mwa miaka 1990 na amelazwa mara kadhaa kwa maradhi yanayohusiana na matibabu ya saratani hiyo

1640503134721.jpeg
Askofu Desmond Tutu wakati wa uhai wake

“Kifo chake kimefungua ukurasa mpya wa majonzi na kuongeza idadi ya mashujaa waliofariki walioipigania nchi yetu na Afrika kwa ujumla na tutaendelea kumkumbuka” amesema Rais Cyril Ramaphosa.

Rais Cyril Ramaphosa akiwa na Askofu Tutu enzi za uhai wake.

Taarifa za familia ya Tutu zinamuelezea kwa sentensi moja kama “mtu alietumia matatizo yake kama njia ya kufundisha jamii jinsi ya kujali shida na matatizo ya wengine”

“Alitaka Dunia ifahamu kuwa anasumbuliwa na Kansa ya tezi dume na mtu akiwahi kugundulika anatibiwa na kupona.”

1640503750581.png

Tutu ndiye alieanzisha msemo wa “Rainbow Nation” akimaanisha taifa lenye upinde wa rangi ya mvua wakati ambao Hayati Nelson Mandela akiwa Raisi wa Kwanza mweusi nchini Afrika Kusini.

Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1984 kwa kuongoza kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini

Waziri wa Afya Zanzibar apata dalili za Corona
Wasafiri wa nje ya nchi wapewa masharti mapya