Kikosi cha Azam FC kitaweka Kambi katika Kisiwa cha El Gouna-Misri kwa ajili ya kujiandaa na Msimu Mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Klabu hiyo yenye maskani yake makuu Chamazi-Dar es salaam Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ amethibitisha rasmi taarifa za kikosi chao kuwa na mpango wa kuweka kambi nchini Misri.

Zakazakazi amesema mipango ya maandalizi ya kuelekea Kambini El Gouna-Misri inaendelea vizuri, na Benchi la Ufundi limeridhishwa na mazingira ya kambi hiyo.

“Azam FC inatangaza rasmi kwamba itakwenda ya nchini Misri kwenye maandalizi ya msimu mpya (Pre-Season), timu yetu itaweka kambi katika mji wa Elguna ambao upo kisiwani”

“Huu mji ni wa kitalii na una mandhari nzuri ya kupendeza ambayo itawasaidia wachezaji wetu wawe na hali nzuri na mazingira ya kuvutiwa kujiandaa na msimu mpya, ambao tumedhamiria kufanya vizuri, tofauti na misimu iliyopita.” Amesema Zakazakazi

Msimu uliopita Azam FC iliweka kambi ya maandalizi nchini Zambia ikiwa chini ya Kocha George Lwandamina ambaye hakubahatika kumaliza msimu, kutokana na kusitishiwa mkataba huku nafasi yake ikichukuliwa na Kocha Abdi Hamid Moallin.

Ndoa ya Kagera Sugar, Nurdin Barola yavunjwa rasmi
Wydad Casablanca kumlipa Mabilioni Simon Msuva