Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Kalimangonga Ramadhan Mtoro Ongala, amekiri kusikitishwa na mwenendo wa kikosi chake, ambacho mwanzoni mwa msimu huu kilikuwa na matumaini makubwa ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Matumaini ya Azam FC kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2022/23 yalizimwa na Ihefu baada ya juzi Jumatatu (Machi 13) kuwatungua bao 1-0 Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.

Kichapo hicho kinaifanya Azam FC kusalia na alama zake 47 baada ya kucheza michezo 25 wamebakiwa na michezo mitano ambayo ni alama 15 ambazo hata ikitokea wakashinda zote hawatawakuta vinara Young Africans wenye alama 65.

Kocha Kally amesema hakutarajia kilichowakuta katikamchezo dhidi ya Ihefu FC, lakini kilichotokea kimewaumiza na hana budi kushirikiana na Benchi la Ufundi watahakikisha kuwa wanafanya maboresho ili hali hiyo isijirudie tena.

“Inasikitisha sana kuona wachezaji wangu wakicheza kwa hali ya chini kiasi kile hasa katika michezo ya ugenini ambayo tumekuwa tukipoteza zaidi.”

“Ligi inasimama kupisha michuano ya kimataifa na kwa upande wetu sisi hatutopumzika, tutakuwa mazoezini kuhakikisha kuwa tunafuta kila aina ya matatizo ambayo yamejitokeza kwenye michezo yetu iliyopita na hatutopumzika hadi ligi itakaporejea.”

“Tukirejea tena kwenye ligi kila mchezo tutakaocheza kuanzia Coastal Union na nyingine zilizobaki tutakua tunakusanya alama tatu tu mpaka ligi iishe.” amesema Kocha Kally

Dada aliyedhihakiwa mtandaoni akiomba kibarua achangiwa Fedha
Simba SC yamkataa Ibourahima Sidibé