Dada mmoja, Mensah Esther Omo ambaye anajishughulisha na biashara ya kuwanunulia watu mahitaji ya nyumbani kuwapelekea katika makazi yao, amejikuta katika mshangazo baada ya watu tofauti kumchangia fedha kutokana na dhihaka aliyofanyiwa na mrembo wa mtandao wa Kijamii nchini Nigeria.

Tukio hilo limemtokea Machi 14, 2023 jijini Abuja, wakati akipitia kurasa mbalimbali za kijamii kutafuta wateja na kuweka tangazo la huduma yake kwenye mjadala wa wafuasi mbalimbali na mrembo huyo, B.G.M ama riterallyrae wa Tweeter alimjia juu kwa kumtukana na kumuonya asithubutu kuweka tangazo lake kwenye ukurasa wake.

Mensah Esther Omo.

Kufuatia hatua hiyo, Esther aliomba radhi na muda mchache mjadala ukaanza kupinga alichokifanya mrembo huyo, wakimlaumu na kumsema kwa tabia mbaya aliyoionesha kwa mtu anayejitafutia riziki halali pasipo kuvunja sheria, huku wakimuomba Esther namba yake ya Akaunti ya Benki, ili wamchangie.

Kwa haraka, Esther akaweka namba ya Akaunti yake kwenye mjadala huo na baadhi ya watu walianza kutuma picha zikionesha risiti ambazo tayari wengi wa wafuasi wa mrembo huyo aliyemkashifu Esther walikuwa wamemuingizia pesa na kuifanya siku yake kuwa ya mshangazo huku akimshukuru MUNGU na zoezi hilo bado linaendelea.

Kamishna wa Uhifadhi TAWA ala kiapo cha utumishi
Azam FC yakubali yaishe Ligi Kuu 2022/23