Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm ameeleza kuwa ushindani wao dhidi ya Azam FC kwenye kumaliza nafasi ya tatu umewafanya wasitishe masuala ya usajili kwa sasa mpaka watakapomaliza ligi kabisa.

Singida Big Stars ipo nafasi ya nne na alama 54, Azam FC ni ya tatu kwa alama 56 huku ikiwa imesalia mechi moja kuhitimisha Ligi Kuu Bara msimu huu.

Pluijm amesema wanahitaji kuimarisha timu kwa ajili pia ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao lakini kwa sasa wanatazamia kumaliza vizuri ligi kisha wageukie mchakato huo aliodai unahitaji umakini mno kulingana na michuano iliyo mbele yao msimu ujao.

“Mwisho wa msimu tukimaliza kabisa hesabu za ligi ambapo siku si nyingi tutakamilisha hilo basi nitageukia moja kwa moja sasa kwenye mambo ya usajili, kuhakikisha tunajiweka sawa kwa msimu ujao,” amesema Pluijm.

Dkt. Yonaz apongeza maendeleo ujenzi Uwanja wa Mashujaa
Guardiola asifia ujio wa meneja mpya Spurs