Meneja wa Klabu bingwa nchini England Manchester City, Pep Guardiola amesifu ujio wa Meneja Ange Postecoglou kwenye klabu ya Tottenham Hotspur.

Postecoglou alitangazwa kuwa Meneja mpya wa Spurs kwa mkataba wa miaka minne juzi Jumanne (Juni 06) na ataanza kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa Jiji la London Julai Mosi na anakuwa Meneja wa kwanza kutoka Australia kufundisha Ligi Kuu ya England.

Kocha Guardiola na Postecoglou walikutana Julai 2019 wakati Meneja huyo kutoka Australia akiifundisha klabu ya Ligi Kuu ya Japan, Yokohama F.Marinos.

City na Marinos walicheza mchezo wa kirafiki ambao klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilishinda mabao 3-1, lakini Marinos walimiliki mpira kwa asilimia 58.

“Meneja mwingine bora anakuja,” amesema Guardiola kuelekea mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan, ambapo klabu hiyo kutoka England inatazamia kushinda taji hilo.

“Nilikuwa na bahati kukutana naye Tokyo miaka kadhaa nyuma wakati akiwa kocha wa Yokohama, moja ya klabu zetu kwenye City Football Group, na tulikuwa na mazungumzo mazuri.

“Nina mahusiano mazuri na mmiliki wa Celtic na atafanya kazi nzuri kwa Spurs.” Amesema Guardiola

Guardiola alikumbuka ugumu wa timu yake kupata ushindi jijini London hasa dhidi ya Tottenham ambao wamekuwa wakicheza soka la kujihami.

Kutokana na hilo kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya kocha Postecoglou ambaye anapenda soka la kushambulia hataweza kucheza soka la kujilinda kama watangulizi wake.

Azam FC yasitisha usajili Singida Big Stars
Polisi watuhumiwa kushirikiana na Magenge ya uhalifu