Umoja wa wapinzani nchini Kenya umetangaza kusitisha maandamano yaliyopangwa dhidi ya Serikali ili kutafuta njia ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya pande mbili yaliyokwama, kuhusu mvutano unaoendelea.

Wafuasi wa Raila Odinga walifanya maandamano mara kadhaa tangu mwezi kuanza kwa Machi, wakidai uchaguzi wa rais wa mwaka jana uliibiwa, na pia kuilaumu Serikali kushindwa kukabiliana na upandani wa gharama za maisha.

Raila Odinga akiteta jambo na Martha Karuwa. Picha ya NMG.

Muungano wa kisiasa wa Odinga, Azimio la Umoja ulikuwa umepanga kufanya maandamano mengine hii leo Alhamisi Mei 4, 2023, lakini umesema uongozi wake umekubaliana kusitisha mpango huo .

Rais wa Kenya, William Ruto ilitoa wito wa mazungumzo ya pande mbili kujaribu kutatua mzozo huo, lakini mchakato huo ulikwama kutokana na malumbano kadhaa na sasa Azimio imesema imewaita wajumbe wake wa mazungumzo kujadili ushiriki huo.

Ajali mbaya ya Basi iliyouwa abiria na kujeruhi
Meridianbet Watua Buguruni Malapa Kuzindua Duka Jipya