Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Kasesela amesema Baadhi ya Watanzania hawafahamu umuhimu wa Mazingira, na kwamba bado elimu juu ya suala hilo inatakiwa kutolewa ili kuleta ufanisi wa mapambano juu ya utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.

Kasesela, ameyasema hayo wakati akihojiwa na Dar24 kuhusu kila anachokiona katika Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji, linalofanyika mjini Iringa.

Amesema, “Mimi bado sidhani kama wananchi wote wanauelewa juu ya masuala ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira bado elimu inahitajika ili watambue kwamba Mazingira yana maana kubwa kwao maana anayeharibu Mazingira naye anaathirika sasa kama akilijua hili hataweza fanya hivyo.”

Kuhusu uhusika wa siasa na suala la Mazingira, Kasesela ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema vinahusiana moja kwa moja kwakuahata Imani ya CCM inatambua na imeanisha mambo mbalimbali katika masuala ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Wahukumiwa miaka 30 jela kwa ugaidi
Wakandarasi wasiofanya vizuri kukosa miradi