Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Songea imewahukumu watanzania sita kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha vitendo vya kigaidi maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuiangusha Serikali kisiasa na kiuchumi.

Jaji Yose Mlyambina aliyetoa hukumu hiyo alisema washtakiwa hao si tu walikula njama na kushiriki vikao vya kufanya matukio ya kigaidi, wao ndio walifanya matukio ya kigaidi kwa lengo la kuvuruga amani ya nchi.

Katika kosa la kwanza, washtakiwa walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na la pili kifungo cha miaka 30 jela, ila adhabu zote zitatumikiwa kwa pamoja, hivyo watatumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Washtakiwa hao ni Seif Chombo maarufu kwa jina la Baba Fatina na wanaye Abdallah Chombo na Athman Chombo, Mohamed Kamala, Omary Mbonani na Rashid Ally.

Wawili kutua Young Africans Dirisha Dogo
Baadhi ya Watanzania hawafahamu umuhimu wa Mazingira: Kasesela