Mchungaji mstaafu wa kanisa la KKKT, Ambikile Mwasapila maarufu kama ‘Babu wa Loliondo’ aliyekuwa akitoa tiba ya kikombe cha maji ya dawa iliyopata umaarufu mkubwa mwaka 2010, ametoa ushauri wake kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuhusu Afya.

Mchungaji huyo amemshauri rais Magufuli kuangalia kwa kina na kuhakikisha anaboresha huduma hiyo nchini. Alisema kuwa misululu ya watu waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Semunge kwa ajili ya kupata tiba ya kikombe inaonesha namna ambavyo watu wengi wanakabiliwa na matatizo ya kiafya nchini.

“Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano lazima waboreshe huduma za afya. Wananchi wapatiwe uhakika wa tiba bora na nafuu katika maeneo yao,” aliliambia mwananchi.

Katika hatua nyingine, Mzee Mwasapila alieleza kuwa Mungu amempa maono mengine ya kuwepo muujiza mwingine mkubwa utakaovuta umati mkubwa wa watu zaidi ya ule wa kikombe cha dawa hivyo akamuomba rais Magufuli kumsaidia kuboresha miundombinu ya kuelekea katika kijiji hicho.

 

Kigwangalla Awapania Watumishi Watoro, Aeleza Mkakati Wake Hapa
Nape aeleza jinsi ambavyo Radio na TV zitagawana mapato yake na Wasanii kuanzia Januari