Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla ameeleza mkakati wake wa kupambana na watumishi wachelewaji na watoro katika wizara hiyo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Dk. Kigwangalla amesema kuwa anaazimia kukomesha utoro na uchelewaji kazini ili aweke nidhamu ya kazi na uwajibikaji.

“Mimi nitawajibika kazini. Kila mtu atapaswa kuwajibika. Haya ndiyo mahitaji ya wakati huu. Leo nimefungia wachelewaji kazini nje ya geti. Nitaendelea kushughulika na watoro na watorokaji. Nasubiri ripoti ya watendaji kuhusu trend ya watumishi wote watoro, wachelewaji kisha nichukue hatua stahiki! Ili kazi ziende ni lazima tuweke nidhamu ya kazi Na uwajibikaji maofisini.” Dk. Kigwangalla ameandika Instagram.

Mapema leo asubuhi, Dk. Kigwangalla alifika katika ofisi za wizara ya afya jijini Dar es Salaam na kufunga geti ili awanase wafanyakazi waliochelewa kisha akaagiza waliochelewa kuandika barua ya kujieleza.

Yanga Yamuanika Hadharani Issoufou Boubacar Garba
Babu wa Loliondo Amshauri Magufuli Kuhusu Afya, atoa utabiri wa Muujiza Mpya