Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga leo umemtambulisha rasmi raia wa Niger Issoufou Garba.

Utambulisho huo umefanywa na Mkuu ws Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Murro mbele ya waandishi wa habari.

Mapema wiki hii Garba alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu hiyo.

Akizungumza na waandishi ws habari mara baada ya kukabidhiwa jezi namba 14,Garba amesema anafurahi kuichezea Yanga kwani ni timu kubwa.

Aliwaambia wana Yanga hatowaangusha kwa sababu kilichomleta nchini ni kazi ya mpira pekee.

Amepewa jezi namba 14 ambayo kabla yake ilikuwa inavaliwa na beki wa kulia Joseph Zutta aliyesajiliwa kutoka Ghana lakini mkataba wake na klabu hiyo ulivunjwa kwa kile kilichodaiwa ni kushindwa kuonesha kiwango kilichotarajiwa na benchi la ufundi.

Blatter Akiri Kuhisi Machungu Ya Adhabu Ya FIFA
Kigwangalla Awapania Watumishi Watoro, Aeleza Mkakati Wake Hapa