Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blater ambae amesimamishwa kwa muda wa siku tisini kutojihusisha na soka, ametaka kifungo hicho alichofungiwa kwa muda cha kutojihusisha na maswala yote ya soka kufutwa.

Mwanasheria wa kiongozi huyu wa juu wa zamani shirikisho hilo la soka Richard Cullen, amesema ushahidi alionyesha kwamba Blatter alipokuwa ndani ya Fifa hakuwahi kukiuka maadili ya chama hicho.

Wakili huyu alikuwa akizungumza baada ya jopo la maadili la Fifa kusema uchunguzi umefungwa.

Blatter alifungiwa kwa siku 90 kuanzia mwezi oktoba kwa tuhuma za malipo ya dola milioni mbili dhidi ya raisi wa Uefa Michel Platini, ambae pia amefungiwa kwa sakata hilo.

Guus Hiddink Awashiwa Taa Ya Kijani Stamford Bridge
Yanga Yamuanika Hadharani Issoufou Boubacar Garba