Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Argentina na Klabu ya Brighton, Alexis Mac Allister.

Inaarifiwa kuwa pande zote mbili zimeshafanya mazungumzo na kiungo huyo amekubali kufanya kazi na Kocha Jurgen Klopp, wakati suala la mkataba likimaliziwa.

Ingawa kiasi cha usajili wake bado hakijawekwa wazi kwa sasa, lakini thamani halisi ya uhamisho wake unatarajiwa kufikia Pauni 60 milioni.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia, Mac Allister alisaini mkataba mpya na miamba hiyo ya Amex, Oktoba mwaka jana, akiongeza ule wa awali, ambao ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Manchester United Ilidhaniwa kuwa na mpango wa kumsajili kiungo huyo mchezeshaji, lakini iliamua kuachana na hilo baada ya Mac Allister kuonyesha nia ya kwenda Anfield.

DP Word kuleta mageuzi makubwa bandari ya Dar es Salaam
Sanamu ya Mwl. Julius k. Nyerere kujengwa Ethiopia