Mtibwa imebeba pointi tatu za Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Mafunzo kwa bao 1-0.
Kwa wale wa Mtibwa, shukurani watapeleka kwa mshambuliaji Said Bahanuzi aliyefunga bao pekee la mchezo huo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 42 na timu hizo zikaenda mapumziko Mtibwa Sugar ikiwa inaongoza kwa bao moja.
Juhudi za Mafunzo kutaka kusawazisha katika kipindi cha pili, hazikuzaa matunda hata kidogo, hivyo kuifanya Mtibwa kushinda.

Hata hivyo, Mtibwa Sugar haikuonyesha kiwango cha juu sana cha uchezaji ukilinganisha na mechi yao dhidi ya Azam FC ambayo iliisha kwa sare ya mabao 2-2.

Pep Guardiola Avunja Ukimya, Asema Wapi Atakapoelekea
Magufuli afuta hati ya Ardhi ya Mwekezaji na kuwakabidhi wananchi