Daktari wa Simba SC Edwin Kagabo ameshusha Presha za Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo, kufuatia taarifa aliyoitoa kuhusu maendeleo ya Wachezaji Jean Baleke na Pape Osmane Sakho.

Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo ya Msimbazi waliingia Presha, kufuatia wawili hao kupatwa na maumivu wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Hilal ‘Omdurman’ uliopigwa jana Jumapili (Februari 05).

Mshambuliaji Baleke, alishindwa kuendelea na mchezo kipindi cha kwanza baada ya kupata maumivu ya mguu, lakini Sakho alimaliza akiwa anachechemea.

Daktari Kagambo amesema, Wachezaji hao hawakupata madhara makubwa kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo kesho Jumanne (Februari 07) wataungana na wenzao kwenye Programu za mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mabingwa wa Guinea Hoyora AC.

Katika hatua nyingine Daktari Kagambo amesema, Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Augustine Okrah amefanyiwa vipimo vya CT Scan na wanasubiri majibu ili kujua ukubwa wa jeraha lake.

Daktari amesema licha ya kusubiri majibu, bado hana matumaini kama Okrah ataweza kuanza mazoezi hivi karibuni kutokana na kusikia maumivu ya Mguu wake kushoto.

Okrah alikuwa sehemu ya wachezaji walioanza kwenye kikosi cha Simba SC kilichoivaa Al Hilal jana, lakini alishindwa kuendelea na mchezo huo kufuatia maumivu ya misuli.

TPDC yapata ugeni wa Zambia mafunzo Gesi Asilia
CAF: Ruhsa Mashabiki kujaza viwanja