Madiwani katika Mji Mkuu wa Ujerumani, Berlin wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara moja linalompatia heshima Gavana mjerumani wa nyakati za ukoloni katika eneo la Afrika Mashariki Hermann von Wissmann na  kupendekeza kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania.

Barabara ya Wissmannstraße, iliopatiwa jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Straße, jina la aliyekuwa waziri wa kwanza mwanamke Tanzania pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru wa taifa.

Kwa mujibu wa  gazeti la Der Tagesspiegel la nchini Ujerumani,Von Wissman alikuwa gavana wa taifa la Ujerumani Afrika mashariki ambayo kwa sasa ndiyo  Tanzania, Burundi na Rwanda katika mwisho wa karne ya 19 na anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wakaazi wengi.

Kundi la Berlin Postkolonial, mojawapo ya kundi lililohusika na mabadiliko limeunga mkono hatua ya serikali hiyo ya mtaa na limesema kwamba kampeni hiyo ilizuia kuheshimiwa kwa ”Von Wissmann na mahala pake kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi”.

Kila sekunde 100, mtoto 1 aliambukizwa VVU mwaka 2019
NEC yawajibu CHADEMA

Comments

comments