Baraza la Usalama limegawanyika mara baada ya Iran kusema kuwa ina ushahidi wa maandamano ya upinzani yaliyotokea nchini humo kuwa yameratibiwa kutoka nje nchi hiyo, na Urusi imelitaka Baraza hilo kuiacha Iran ishughulike yenyewe na masuala yake ya ndani.
Aidha, hayo yamejiri katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama mjini New York ambacho kiliitishwa na Marekani Ijumaa, kujadili wimbi la maandamano ambalo lilmeitikisa Iran wiki iliyopita.
Hata hivyo, Kikao hicho kilianzia faraghani, lakini baadaye Marekani ilifanikiwa kukifanya kuwa cha wazi licha ya upinzani kutoka Urusi, Ufaransa, Bolivia na baadhi ya wanachama wengine kutaka kuwa cha siri.
-
Mawaziri wawili wakamatwa kwa rushwa
-
Mapigano makali yazuka nchini Misri
-
Video: Rais Magufuli asifu mchango wa Kingunge, Lissu alivyopaa dk 500 Ulaya