Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW limeteketea kwa moto leo Juni 10, 2017 katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama, Mara.

Gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.

Taarifa za awali kutoka kwa waliokuwa abiria wa basi hilo ni kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha isipokuwa baadhi ya mizigo yao imeteketea.

Hadi sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

EXCLUSIVE: Rungwe afunguka kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali, "Imepambwa sana..." (Video)
Kampuni ya Japan yaajiri paka na mbwa kuongeza ufanisi ofisini