Klabu ya Lille Olympique Sporting ya Ufaransa, inajipanga kuwasilisha ofa ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Chelsea Michy Batshuay.

Uongozi wa Lille, unaamini huenda ukafanikisha kumpata mshambuliaji huyo, kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Antonio Conte.

Taarifa zilizochapishwa na mtandao wa La Voix du Nord, zinaeleza mipango ya usajili wa mkopo kwa mshambuliaji huyo, inasukwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, na tayari utaratibu wa kuanza kwa mazungumzo unaandaliwa.

Hata hivyo taarifa hiyo imeendelea kutanabaisha kuwa, ombi la Lille halitojumuisha mpango wa usajili wa moja kwa moja kwa Batshuay, zaidi ya kutaka wawe naye hadi mwishoni mwa msimu huu.

Batshuayi alijiunga na The Blues akitokea Olmypique Marseille kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 33 wakati wa majira ya kiangazi, na mpaka sasa hajabahatika kuanza katika kikosi cha kwanza kwenye michezo ya ligi ya nchini England.

Majaliwa atoa onyo kali kwa wanaokata miti
Young Africans Wakomaa Na Point Za Mezani