Serikali nchini Burundi imekifungia chombo cha habari cha kimataifa BBC kufanya kazi katiaka nchi hiyo, na kuongeza hofu ya vyombo vya habari na waandishi wa habari juu ya uhuru wa vyombo vya habari.

Kabla ya kufikia uamuzi huo jana, Baraza la Taifa la mawasiliano nchini Burundi (CNC), walikuwa wamesimamisha kwa muda matangazo ya redio ya BBC na idhaa ya sauti ya Amerika (VOA) mwezi Mei 2018.

Huku BBC wakiwa wamefungiwa kabisa kuripoti na kunyang’anywa leseni ya utangazaji nchini humo, VOA wao bado wanaleseni na wanaendelea kutumikia adhabu yao ya kufungiwa kwa muda (suspension), na wanahabari wote nchini Burundi wameonywa hawatakiwi kutoa habari kwa BBC au VOA.

“Hairuhusiwi kabisa kwa mwandishi yeyote wa habari hapa Burundi au kutoka nje ambaye ana ripoti taarifa za Burundi kuwapa habari BBC au VOA ili wazitangaze, moja kwa moja au kwanjia nyingine” taarifa ya CNC imeeleza.

Katika uhuru wa habari bila mipaka, Burundi ni nchi ambayo inashika nafasi ya 159 kati ya 180 ambazo zimefanyiwa utafiti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa BBC imekosoa vikali uamuzi huo na kueleza kuwa ni kinyume na haki ya uhuru wa vyombo vya habari na wamelaani kitendo hicho.

“Tunaamini kuwa ni haki ya kila mtu ulimwenguni kupata habari zakujitegemea na zilizo sahihi, pamoja na watu wa Burundi takribani milioni 1.3 nao wanahaki pia ambao kwa sasa wamekuwa wakitegemea sana habari kutoka BBC”

Nchi ya Burundi imekuwa katika migogoro tokea Rais Pierre Nkurunziza abakie madarakani kwa muhula wa tatu mwaka 2015, na kupelekea watu 1,200, kupoteza maisha na wengine zaidi ya 400,000 kupoteza makazi, kwamujibu wa takwimu za kuanzia mwezi April 2015 hadi Mei 217, zilizotolewa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC baada ya kufanya uchunguzi.

Kwa upande wa BBC waliingia kwenye mgogoro na nchi ya Burundi baada ya kuonesha makala inayohusisha askari wakiendeleza genge la siri la mateso ili kudhibiti wananchi, jambo ambalo serikali imelipinga vikali.

Na idhaa ya sauti ya Amerika wao waliingia katika mgogoro na serikali ya Burundi baada ya mtangazaji wao wa redio Patrick Nduwimana anashukiwa kufanya kazi katiaka kikosi cha jeshi mwaka 2015.

Shirika la habari la BBC na VOA wameendelea kurusha matangazo yao kwa masafa mafupi ambayo yanaweza kusikilizwa ndani ya nchi na mtu yeyote aliye na redio.

 

 

 

 

 

Chriss Brown amtaka Eddy Kenzo, Ghetto Kids wimbo wake mpya
Ajifungua mapacha mwezi mmoja baada ya kujifungua mtoto wa kwanza