Bei ya mafuta duniani imeanza kupanda takribani kwa asilimia 6 baada ya muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi, Opec, kukubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane baada ya mafuta kushuka bei kutoka $110 miaka miwili iliyopita.

Ni  Iran pekee itaruhusiwa kuongeza uzalishaji wake.

“Opec imechukua uamuzi wa kipekee leo,” waziri wa mafuta wa Iran Bijan Zanganeh amesema.

Mawaziri wa mafuta wa nchi wanachama wamesema maelezo ya kina kuhusu mwafaka wa sasa yatajadiliwa kwenye mkutano mwingine Novemba.

Uzalishaji wa mafuta utapunguzwa hadi mapipa 700,000 kwa siku, ingawa upunguzaji wa uzalishaji hautakuwa sawa miongoni mwa wanachama.

Kulikuwa na mtafaruko awali baina ya Iran na mpinzani wake Mashariki ya Kati Saudi Arabia, jambo ambalo lilikuwa limezuia kupatikana kwa mwafaka.

Waziri wa mafuta wa Nigeria Ibe Kachikwu, taifa lililoathirika sana, alisema huo ni “mkataba mzuri sana”.

Waziri wa kawi wa Algeria Algerian Noureddine Bouarfaa amesema uamuzi huo huo ulifikiwa kwa kauli moja.

Waziri wa kawi wa Qatar Mohammed Bin Saleh Al-Sada ambaye ndiye rais wa sasa wa Opec amesema uzalishaji sasa utakuwa kati ya mapipa 33.2 milioni na 33 milioni kwa siku.

Uzalishaji wa sasa unakadiriwa kuwa mapipa 33.3 milioni kwa siku.

Taifa Stars Watakaoivaa Ethiopia Hawa Hapa
Selena Gomez avunja rekodi ya Instagram duniani, lakini yamuachia ‘ugonjwa ‘