Mlinda Lango wa Singida Big Stars Benedict Haule amesema kitendo cha kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kwake ni rekodi nyingine ambayo ameiandika katika historia yake ya soka.

Beko msimu huu ameifikisha Singida Big Stars kwenye Nusu Fainali na juzi Jumapili (Mei 21) ikatolewa dhidi ya Young Africans kupitia bao lililofungwa na Fiston Mayele dakika ya 82.

Beko amesema alitamani kufika fainali ya kombe hilo na Singida BS, kwani tayari alishafanya hivyo wakati akiichezea Mbao FC.

“Kama Mchezaji nilitamani nifike kwenye hatua ya fainali ili nitengeneze rekodi nyingine, si mbaya hata kwa hapa nilipoishia kwa sababu nayo ni sehemu ya historia kwangu.

“Maendeleo yangu ni mazuri na nikiwa kama mchezaji najivunia kujiona kadri siku zinavyozidi kusonga mbele naimarika na kuwa kwenye wakati mzuri ndani ya uwanja,” amesema Mlinda Lango huyo

Beko pia amehakikisha anakuwa bora langoni na timu hiyo kuwa nafasi ya nne kwenye ligi hadi sasa na kujihakikishia kushiriki kimataifa msimu ujao.

Pia, aliwahi kuwa langoni akiwa na Mbao FC kwenye fainali ya Kombe la ASFC, wakati timu yake ikifungwa na Simba 2-1.

Viongozi 10 waliozibeba nchi zao Afrika – 3, Kwame Nkrumah 1
Tume ya uchunguzi mauaji ya Shakahola yapigwa stop