Benki ya ABC nchini imezindua ofa kabambe kwa wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ambapo wateja wapya wanaofungua akaunti maalumu watapata riba ya riba hadi 16% kulingana na kiasi cha amana watakachoweka.

ABC imezindua ofa hiyo Desemba 6, 2016 Jijini Dar es Salaam ambapo wateja watakao fungua akaunti ya amana na kuweka pesa kuanzia milioni 10 kwa muda maalum atafaidika na ofa hii yakupata riba ya juu kuliko zote hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na wafanya biashara wadogo wa benki hiyo, Joyce Malai amesema wanatoa riba ya hadi 16% kwa mwaka na kwamba watalipwa riba papo kwa papo ikiwa ni zawadi yao msimu huu wa sikuku.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko na Fedha, Barton Mwasamengo amesisistiza kuwa lengo la benki hiyo ni kufikia mahitaji ya wateja na kuhakikisha kwamba wanakua pamoja na benki hiyo kila siku.

“Tunathamini jinsi wateja wetu wanavyotuunga mkono na hiyo ndio sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe katika msimu huu wa sikukuu,” alisema.

“Kinachotakiwa kufanywa na mteja yeyote ili aweze kujipatia ofa hii nikufika kwenye tawi letu lolote – Uhuru, Quality Centre, Kariakoo na Arusha, afungue akaunti ya amana ya muda maalumu ambapo riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kukupa uhuru wa kuitumia kwa ajili ya kufanya manunuzi binafsi kama upendavyo ikiwemo kununua zawadi kwa familia au marafiki ili kuwaongezea furaha katika msimu huu wa sikukuu,” alisema.

Ofa hiyo itawahusu wateja watakaofungua akaunti za amana za muda maalumu na Benki ya ABC kabla ya Desemba 31 mwaka huu pekee.

examination: prime service to obtain paper on any topic swiftly & with no trouble
Professional review of Custom Writing Company with regard to College Students