Beyonce ameuanza mwaka mpya kwa kuifumua timu yake ya ushindi iliyokuwa ikisimamia kazi zake za muziki.

Mwimbaji huyo amemfuta kazi meneja wake aliyefanya naye kazi kwa kipindicha miaka 10, Anne Callahan-Longo na nafasi yake imechukuliwa na Steve Pamon.

Pamon aliwahi kufanya kazi kama kiungo kwenye timu ya mwimbaji huyo mwaka 2014 wakati wa ziara yake kubwa ya dunia akiwa na mumewe Jay Z, ‘On The Run Tour’.

Fagio hilo la Queen Bey limewafagia wafanyakazi wengine wa timu yake akiwemo ndugu yake na sasa ameajiri watu wapya kabisa.

Hii inaweza kuwa ni hatua nyingine ya Beyonce kutaka kuhakikisha kuwa anapambana na ushindani mkali uliopo hivi sasa, uliomfanya ategee kuachia albam yake akiisubiri nyota ya albam ya ‘25’ ya Adele itulie.

“Beyonce amefagia nyumba, ameitimua timu yake yote ambayo ilikuwa ikimjumuisha ndugu yake na sasa ameajiri timu mpya. Anataka kuzungukwa na watu wanaojua biashara wanaoweza kuupandisha ngazi zaidi muziki wake.

Hii ni hatua nyingine kubwa aliyowahi kuichukua Beyonce, mwaka 2011 alimtimua kazi baba yake mzazi, Mathew Knowle aliyekuwa meneja wake tangu alipoanza muziki.

Lowassa aweka mezani walichozungumza na Waziri Mkuu Majaliwa
Magufuli aahidi kuendeleza 'minyoosho', asema yeye sio kichaa, Dikteta