Zaidi ya wajasiriamali 225,000, wamenufaika na mikopo ya Kilimo tangu kuanzishwa kwa mfuko wa Self Microfinance Fund, ambapo jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 313 kimetolewa.
Hayo yamebainishwa jijini Dodomana Meneja Masoko na Uhamasishaji wajasiriamali wa mfuko huo, Linda Mshana katika warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari.
AAmesema, urejeshaji wa mikopo hiyo umekuwa ukiridhisha kwa asilimia 93 hali iliyosababisha mtaji kukua kutoka bilioni 62 hadi kufika zaidi ya bilioni 300, tangu kuanzishwa kwa mfuko huo.
Linda ameongeza kuwa, dhumuni la Self Microfinance Fund ni kuhakikisha inatoa mikopo ili kuwawezesha kukidhi mahitaji ya kifedha na kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya kilimo na pembejeo kwa wakulima na wafugaji.
Aidha, pia wamejipanga kuhakikisha asasi zenye kutoa mikopo zinajengewa uwezo wa kuhudumia wakulima na Wajasiriamali wenye uhitaji wa kifedha, katika shughuli za kilimo.