Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) amesema mpaka sasa vijiji 8,708 kati ya 12,327 vinapata huduma ya majisafi na salama nchini kwa sasa.

Amesema kukamilika kwa miradi 1,139 ya maji vijijini ambapo jumla ya Sh. bilioni 688.81 zimetumika kuboresha huduma ya maji vijijini na kumeongeza wastani wa upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka asilimia 64.8 mwaka 2019 hadi 72.3 kifikia mwezi Juni, 2021.

Aidha, Waziri Aweso amesema katika wastani wa wakazi wa mijini wanaopata huduma ya majisafi na salama imeongezeka kutoka asilimia 25 kwa wakazi wote wanaoishi mijini mwaka 1961 hadi kufikia wastani wa asilimia 86 mwaka 2021.

Akitoa taarifa ya mafaniko ya Sekta ya Maji katika miaka 60 ya Uhuru, Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji imetenga Sh. bilioni 139.4 kutekeleza miradi 218 nchini kote ikiwa ni sehemu ya mikakati ya wizara kuimarisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi.

IGP Sirro afanya mabadiliko ya makamanda wa Polisi
PICHA: Kocha Franco atinga kambini