Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Helen Kijo-Bisimba amesema kuwa ongezeko la migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji linatokana na baadhi ya viongozi wa serikali kushindwa kutafuta suluhisho la kudumu.

Aidha, Bisimba amesema kuwa hakuna mpango wa ufuatiliaji matatizo ya ndani ambayo yanahitaji ufumbuzi ya migogoro ya ardhi.

“Tatizo la migogoro hii ya ardhi bado ni kubwa, na linakuwa kutokana na serikali haijaweza kutafuta suluhisho la kudumu la ardhi,mara nyingi tatizo hilo linatokana na kuwa na maeneo madogo hali ambayo wafugaji hulazimika kuingia kwenye maeneo ya wakulima na hivyo kuibua migogoro,”amesema Bisimba.

Aidha, amesema ili kumaliza tatizo hilo ni vema serikali ikatenga maeneo ya wafugaji ili kuepusha kuzunguka na mifugo yao na kuwaacha wakulima na maeneo yao.

Chadema yatoa siku saba kwa DC kurejesha misaada yao
Lowassa atoa neno kwa waliomtabiria kifo