Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), wametoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama kurejesha mabati 850 kiliyotoa kwaajili ya waathirika wa tetemeko la mwakata.

Wametoa tamko hilo siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, kusema kuwa serikali haitawajibika kumjengea mtu nyumba aliyeathirika na tetemeko Mkoani Kagera kwa kuwa si jukumu lake,bali kila mtu atabeba msalaba wake.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya hiyo Juma Ntahimpeta,amesema chama chake kilitoa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 12, kusaidia wakazi wa mwakata ili kupata makazi mapya.

“Sasa kwa sababu serikali ya CCM imesema haijengei mtu,na sisi chadema tunajua waathirika bado wapo,na kwa sababu tulitoa msaada kwaajili ya kujengea watu makazi, DC wa Kahama rudisha mabati ya Chadema tukayagawe sisi wenyewe,”amesema Ntahimpeta.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu amesema walisha mwandikia barua juu ya kurejesha msaada huo naye akawajibu kwa barua kuwa kama wana vielelezo vya barua kuwa walitoa msaada huo atawarejeshea.

Gambo kumaliza migogoro yote Arusha
Bisimba: Serikali chanzo cha migogoro ya ardhi