Nahodha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC John Raphael Bocco ameachwa jijini Dar es salaam, licha ya kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars), kilichoingia kambini mwishoni mwa mwezi Agosti kujiwinda na mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la dunia 2021 dhidi ya DR Congo.

Mshambuliaji huyo ameachwa kufuatia kuwa majeruhi, na huenda akatumika kwenye mchezo wa pili wa kuwania kufuzu dhidi ya Madagascar, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili jijini Dar es salaam.

Kuachwa kwa Mshambuliaji huyo kutamuwezesha Kocha Mkuu Kim Poulsen kuwatumia Simon Msuva na Mbwana Samatta ambao watacheza pamoja eneo la ushambuliaji.

Stars inatakiwa kupambana na kushinda mchezo dhidi ya DR Congo, ili kufanikisha mwanzo mzuri wa safari ya kushiriki Fainali za Kombe la dunia mwaka 2022, zitakazounguma nchini Qatar.

Tanzania imepangwa kundi J na timu za DR Congo, Benin na Madagascar.

Kamwaga: Sitaongeza muda Simba SC
Hatma kesi ya Mbowe kujulikana leo