Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) itafanya Mkutano wake wa Pili wa Baraza Kuu (Governing Council) jijini Dar es Salaam, Jumapili, Desemba 13 mwaka huu.

Mkutano huo utahudhuriwa na Marais/Wenyeviti wa klabu zote 40, ambapo 16 ni za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine 24 za Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes na kutoa mwelekeo wa Bodi kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ndiye anayetarajiwa kufungua Mkutano huo utakaofanyika kuanzia saa 10 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa Taifa.

40 Waswekwa Rumande Sakata La Makontena
Rais Wa TFF Ampongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo