Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), Dk Cosmas Mwaisobwa amesema hivi karibuni wanatarajia kutangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia mikopo wanafunzi elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

”Tunakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai tuwe tumeutangaza na tumefungua mtandao wetu ili waombaji wenye sifa waombe”.

Hivyo amewathibitishia waombaji wa mkopo kuwa wakati wowote kuanzia mwezi huu sifa za waombaji zitawekwa wazi na mikopo itatolewa kwa kuzingatia vigezo hivyo.

Aidha amewaomba wanafunzi wote waombaji wa mikopo hiyo wawe watulivu na kufuatilia kwa ukaribu vyombo vya habari na tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).

Zaidi amechukua nafasi hiyo kuwakumbusha wadaiwa na walionufaika na mkopo huo wa masomo elimu juu kuanza kurejesha mkopo hiyp ndani ya miezi 24 mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Waziri wa Usalama Kenya Joseph Nkaissery afariki dunia, Lowassa atoa neno
Ripoti ya PAC yaanika vigogo, wanasiasa na viongozi wa dini upigaji hela za Escrow