Shirika la Ndege Tanzania,(ATCL) linatarajia kutumia ndege zake mpya kufanya safari zake katika nchi za Afrika Mashariki na Mashariki ya mbali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi, amesema kuwa hatua hiyo itafikiwa baada ya kuwasili kwa ndege mpya mbili aina ya Bomberdier CS300 kutoka nchini Canada mwaka 2018 ambazo zitakuwa na uwezo wakubeba abiria 160 kila moja.

“Teyari zimeshaagizwa na mazungumzo yamesha fanyika na tumefikia makubaliano, hivyo kinachosubiliwa ni kuwasili tu kwa ndege hizo hapa nchini”amesema Matindi.

Aidha amebainisha kuwa ndege hizo ya kwanza itawasili kuanzia juni hadi julai na pili kuwasili Septemba 2018, ambapo aliweka wazi kuwa ndege hizo ni kubwa zaidi ya zile zilizo wasili awali na kwamba zinatumia jet engine na si plopera au pangaboi kama ndege zingine.

Hata hivyo, Matindi amesema kutokana na ujio wa ndege hizo shirika hilo linatarajia kuongezeka na kupanuka kwa huduma za usafirishaji kwenda nchi mbalimbali za Afrika mashariki na kati

Samia Suluhu kuzindua mpango kazi kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake
Video: Dangote awaibua wasomi kwa JPM, Miili kwenye viroba yamuibua Mwigulu...