Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inadaiwa na Wafanyakazi waliofukuzwa  katika benki hiyo mwaka 1993, ambapo  wamechukua hatua mpya mara baada ya  kuwasilisha madai ya malimbikizo ya mishahara yao  yanayofikia sh 3.5 bilioni  na kutaarifu kuwa watarejea kazini  kuanzia Januari 2, 2017.

Aidha madai hayo ni ya kipindi cha kuanzia Januari 1996 hadi Desemba 2011, ambapo wafanyakazi hao wamewasilisha madai hayo mara baada ya jaribio la BoT kupangua hukumu iliyowapa ushindi katika kesi yao ya kupinga kupunguzwa kazini.

BoT iliwaondoa kwenye ajira ya wafanyakazi  hao mwaka 1993 wakati Serikali ikitekeleza mpango wake wa kurekebisha taasisi za umma kwa kupunguza wafanyakazi kwenye sekta hiyo.

Hata hivyo wafanyakazi  hao wameongozwa na Samson Magoti, Mbaraka Katundu, Fabian Nguyeje, Omari Hassan na Alfonsi John. katika kupigania maslahi yao.

Majaliwa ageukia malipo ya wakulima
Waziri Mkuu avipa ‘Tano’ vyombo vya habari Mwaka mmoja wa JPM