Mabingwa wa Afrika mwaka 2017, timu ya taifa ya Cameroon wamepanda kwa nafasi 29 kwenye viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Februari.

Cameroon ambao waliifunga Misri mwishoni mwa juma lililopita mabao mawili kwa moja, katika mchezo wa hatua ya fainali ya AFCON uliochezwa mjini Libreville nchini Gabon, kwa sasa wanashika nafasi ya 33 duniani.

Mwezi uliopita taifa hilo la Afrika ya kati lilikuwa linakamata nafasi ya 69.

Kwa upande wa viwango vya ubora wa soka barani Afrika, mabingwa hao mara tano wa AFCON wamepanda kwa nafasi tisa, wakitoka katika nafasi ya 12 hadi nafasi ya tatu.

Makamu bingwa wa AFCON 2017, timu ya taifa ya Misri wapo katika nafasi ya 25 wakiwa wamepanda kwa nafasi 12, ambapo kwa mwezi uliopita walikua nafasi ya 37.

Wana robo fainali katika michuano ya AFCON kwa mwaka huu, timu ya taifa ya Senegal, ambayo kwa mwezi uliopita ilikamata nafasi ya kwanza barani Afrika, wameshuka hadi nafasi ya pili na upande wa dunia wanashika nafasi ya 31.

Ifuatayo ni orodha ya timu zilizoshika nafasi kumi bora upande wa bara la Afrika, kufuatia viwango vya ubora wa soka duniani ambavyo vimetolewa hapo jana.

1 (3) Egypt, 2 (1) Senegal, 3 (12) Cameroon, 4 (4) Tunisia, 5 (6) DR Congo, 6 (8) Burkina Faso, 7 (7) Nigeria, 8 (9) Ghana, 9 (2) Ivory Coast, 10 (10) Morocco.

Muhimu: namba zilizopo kwenye mabano ni nafasi kwa timu husika kwa mwezi uliopita.

Wakati huo huo upande wa viwango vya ubora wa soka duniani, timu ya taifa ya Argentina inaongoza, ikifuatiwa na Brazil huku mabingwa wa soka duniani kwa sasa timu ya taifa ya Ujerumani wakishika nafasi ya tatu.

  1. Chile, 5. Belgium, 6.Ufaransa, 7. Colombia, 8. Ureno, 9. Uruguay, 10. Hispania, 11. Uswiz, 12. Wales, 13. England, 14. Poland, 15. Italia, 16. Croatia, 17. Mexico, 18. Peru, 19. Costa Rica, 20. Iceland.

Katika viwango hivyo Tanzania imeanguka kwa nafasi mbili ikitoka nafasi ya 156 hadi 158.

Cheick Tiote Atimkia China
Tundu Lissu akiri alichokisema