Chama cha Mapinduzi (CCM) kimezungumzia hoja zilizotolewa na baadhi ya watu kuwa baraza la Mawaziri lililotangazwa hivi karibuni na rais John Magufuli halina uwakilishi wa kutosha kutoka Zanzibar.

Akizungumzia hoja hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai alisema kuwa baraza hilo limetoa mgawanyo wenye mantiki kwa pande zote mbili kutokana na udogo wa baraza lenyewe.

“Kwanza baraza hili ni dogo ukilinganisha na baraza lililopita. Sasa mimi sina uhakika kwamba wanaosema kuwa baraza hili linauwakilishi mdogo wanatumia vigezo gani,”alisema Vuai.

Alifafanua kuwa baraza lililopita likuwa na mawaziri takribani 60 huku baraza hili litakuwa na jumla ya mawaziri na manaibu waziri 34 tu hivyo mahesabu yanapaswa kuzingatia ukubwa wa baraza lililopita na baraza la wakati huu.

Aliongeza kuwa ni vyema kusubiri hadi pale ambapo rais atakapomaliza uteuzi wa mawaziri wanne waliosalia ili kuweza kuzungumzia mgawanyo huo.

“Lakini bado baraza hili halijakamilika, kuna nafasi bado hazijajazwa. Bado… tusiwe na haraka ya kufanya maamuzi kwamba labda uwakilishi wetu ni mdogo,”alisema.

Jose Mourinho Abaini Madudu Yanayoitafuna Chelsea
Kilichojiri Baada Ya Vigogo Wa TRA Wa Makontena Kuomba Dhamana Mahakama Kuu