Baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amedai kuwa wachezaji wanamsaliti

Mourinho amesema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka kidedea lakini imeshindikana.

Amesema moja ya vipawa vyake ni uwezo wa kusoma na kuelewa mchezo kwa haraka, lakini kwa hilo anahisi amesalitiwa.

Amesema wakati mwingine anahisi kama vile alijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji wake msimu uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika kiwango hicho.

Msimu uliopita Chelsea walipoteza katika mechi tatu tu walizoshiriki lakini msimu huu, mambo yamewageuka na maji yamezidi unga.

The Blues sasa wapo katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zilizo kwenye hatari ya kushuka daraja msimu ujao.

Hata hivyo kinachomkera sana raia huyo wa Ureno ni kichapo cha 2-1 mikononi mwa vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City.

Dar es salaam Young Afrcans Wamalizana Na Paul Nonga
CCM Yajibu hoja kuwa baraza la Mawaziri linaipunja Zanzibar