Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa onyo kwa wafuasi wa vyama vyote vya siasa kuhakikisha wanafuata maagizo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kurudi majumbani baada ya kupiga kura, Chadema kimemlalamikia rasmi kwenye Mahakama ya Kimataita ya Makosa ya Jinai (ICC) na Umoja wa Mataifa.

Akiongea na waandishi wa habari jana jiji Dar es Salaam, mwanasheria wa Chadema, John Mallya alisema kuwa wamemshtaki rais kwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika pamoja na Mahakama ya Makosa ya Jinai (ICC- The Hugue), kwa kile walichodai kutumia vibaya madaraka na kutoa kauli za vitisho kuelekea uchaguzi mkuu.

Mwanasheria huyo ameeleza kuwa barua hiyo ya mashtaka ambayo nakala yake imetumwa kwa Umoja wa Afrika (AU), imesainiwa na Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari.

Chadema pamoja na vyama vinavyounda Ukawa wameendeelea kuvutana na Tume ya Uchaguzi na Serikali kuhusu kukaa mita 200 baada ya kupiga kura, huku serikali na Tume wakisisitiza wananchi kurudi majumbani mara tu baada ya kupiga kura.

 

Ukawa Wasitisha Kampeni Saa 24 Kumuaga Dkt. Makaidi
TFF Yatajwa Kuwa Chanzo Cha Upinzani Ligi Kuu