Vyama vya Upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimetangaza kusimamisha kampeni zake nchi nzima kwa saa 24 kujumuika pamoja kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi.

Mwili wa Dkt. Makaidi unaagwa leo majira ya saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam na kisha kuzikwa katika makaburi ya Sinza.

 “Baada ya kumuaga shujaa wetu pale Karimjee tutaenda kumzika katika makaburi ya Sinza. Kampeni zetu zitaendelea tena kama kawaida siku ya Jumatano wakati mgombea wetu wa urais atakapokuwa Morogoro,” alisema mkuu wa Idara ya Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene.

Dkt. Emmanuel Makaidi alikuwa mwenyekiti wa NLD iliyokuwa moja kati ya vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, alikuwa mgombea ubunge wa jimbo la Masasi.

Kada Mwingine Aihama CCM Dakika Za Lala Salama
Chadema Wamshitaki Rais Kikwete Umoja Wa Mataifa Na ICC