Klabu ya Chelsea imewasilisha rasmi ofa ya kutaka kumsajili beki kutoka nchini Ufaransa na klabu ya SSC Napoli ya Italia, Kalidou Koulibaly.

Gazeti la The Telegraph limeripoti kwamba, The Blues wametuma ofa ya Pauni milioni 34, ambazo wanaamini zitatoa ushawishi kwa viongozi wa SSC Napoli ili kukubali kumuachia beki huyo mwenye umri wa miaka 25.

Chelsea walianza kumfuatilia, beki huyo mzaliwa wa nchini Senegal, tangu waliposaini mkataba na meneja mpya kutoka Italia Antonio Conte, lakini walionyesha kusita kufanya maamuzi ya kutuma ofa ya kumsajili.

Conte, anaamini usajili wa beki huyo kama utakamilishwa kutakua na muamko tofauti katika safu yake ya ulinzi ambayo kwa sasa inaongozwa na John Terry akisaidiana na Garry Cahill, huku Kurt Happy Zouma akiendelea kuuguza majeraha ya mguu.

Leonardo Bonucci

Hata hivyo Chelsea wamejipanga kuwasilisha ofa kwa ambingwa wa soka nchini Italia, Juventus kwa ajili ya usajili wa beki Leonardo Bonucci, endapo watashindwa kumsajili Koulibaly.

Mancini Kuingia Kwenye Kinyang'anyiro cha Ukocha Wa England?
Juventus FC Wafanya Kweli Kwa Alexis Sanchez