Wachezaji Diego costa na Eden Hazard usiku wa kuamkia leo waliiwezesha Chelsea kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini England, baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya West Ham Utd.

Chelsea walikuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za West Ham Utd katika dakika ya 25 kipindi cha kwanza kwa bao la Eden Hazard, baadae Diego Costa akawachapa The Hammers bao la pili na la mwisho katika dakika ya 50.

West Ham United walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Manuel Lanzini dakika ya 90.

Kwa ushindi huo Chelsea wamefikisha point 66 na kuiacha Tottenham iliyo nafasi ya pili kwa point 10, huku Man city, Liverpool, Arsenal na Manchester United zikijikongoja kwa mwendo wa kinyonga.

Ushindi huo kwa Chelsea ni dalili nyeupe ya kutwaa taji la ligi kuu England msimu wa 2016/17, kwa kuwa hakuna dalili za timu yoyote kuweza kufikisha idadi ya point ambazo tayari Chelsea wamejikusanyia.

Katika timu ambazo zimeonyesha njia ya kushuka daraja kwa kuwa na point chache kuliko timu zote ni Sunderland wanaoburuza mkia kwa kuwa na point 19, wakifuatiwa na Hull City wenye point 21 na Midllesbrough wenye point 22.

Trump aendelea na msimamo wake kuhusu wahamiaji
Video: Wagonjwa dawa za kulevya waongezeka