Mkurugenzi wa Tiba kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Edwiga Swai amesema kuwa waathirika wa dawa za kulevya wameongezeka  kutoka watu watano kwa siku hadi 25.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, amesema kuwa idadi hiyo imeongezeka kutokana na kamata kamata ya operesheni inayoendelea ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba inayoendelea nchini.

Aidha, amesema kuwa idadi hiyo ya wagonjwa imeongezeka kutokana na bidhaa hiyo kuadimika hivyo kuwafanya watumiaji kuwahi kwenye matibabu ili kuweza kujinusulu na matatizo mengine.

Chelsea Waendeleza Moto Wa Ushindi
Jenifer: Nilionekana wa ajabu kwa walimu na wanafunzi