Ligi kuu ya soka nchini England iliendelea tena usiku wa kuamkia hii leo kwa michezo kadhaa kuchezwa, ambapo vinara Chelsea walikua nyumbani kwa Sunderland (Stadium Of Lights) wakisaka point tatu muhimu.

Bao la kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas, lilitosha kuwapa ushindi The Blues na kujikita kileleni kwa tofauti ya point sita dhidi ya wapinzani wao.

Ushindi huo kwa Chelsea unakuwa wa kumi mfululizo, hali ambayo inaendelea kudhihirisha ubora wa kikosi kinachonolewa na meneja kutoka nchini Italia Antonio Conte.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya nchini England iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Middlesbrough 0 – 3 Liverpool

West Ham United 1 – 0 Burnley

Crystal Palace 1 – 2 Manchester United

Manchester City 2 – 0 Watford

Stoke City 0 – 0 Southampton

Tottenham Hotspur 3 – 0 Hull City

West Bromwich Albion 3 – 1 Swansea City

 

Zola Arithishwa Mikoba Ya Gary Rowett Birmingham City
Chadema watoa tamko kuhusu kupotea kwa msaidizi wa Mbowe