Klabu ya Chelsea imeweka Rekodi ya usajili nchini England, baada ya kukamilisha usajili wa Kiungo kutoka Argentina Enzo Fernandez, akitokea Benfica ya Ureno.

Chelsea imeripotiwa kutumia kiasi cha Pauni Milioni 105, kama ada ya usajili wa Kiungo huyo, ambaye walimuwinda wakati wote wa Dirisha Dogo la Usajili, kwa kutuma ofa mara kadhaa.

Imefahamika kuwa The Blues walikubali Dili hilo la Pauni Milioni 105 saa kadhaa kabla ya kufungwa kwa Dirisha Dogo la Usajili usiku wa kuamkia leo, baada ya ofa yao ya Pauni Milioni 100 kukataliwa.

Kwa Mantiki hiyo Klabu ya Chelsea inavunja Rekodi ya usajili iliyowekwa na Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, wakati wakimsajili Jack Grealish mwaka 2021, akitokea Aston Villa.

Usajili huo uliigharimu Manchester City kiasi cha Pauni Milioni 100, ambacho kiliweka Rekodi ya kipekee nchini England, kabla Rekodi hiyo kuvunjwa usiku wa kuamkia leo kwa usajili wa Enzo Fernandez, mwenye umri wa miaka 22.

Ikumbukwe kuwa Enzo Fernandez alikuwa sehemu ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Argentina kilichotwaa Ubingwa wa Dunia nchini Qatar mwaka 2022, huku akiacha kumbukumbu ya kuitumikia Benfica katika michezo 17 na kufunga bao moja.

Jorginho: Arsenal ilishindwa kunisajili
Usajili wa Hakim Ziyech wakwama