Dili la Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Morocco Hakim Ziyech la kusajiliwa kwa mkopo na Klabu ya Bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain limegonga mwamba.

Kiungo huyo tayari alikuwa ameshaanza mazungumzo binafsi na maafisa wa PSG jana Jumanne (Januari 31), lakini uhamisho wake ulikwama kufuatia baadhi ya nyaraka za Chelsea kutokidhi taratibu za usajili.

Chelsea ilidhamiria kumpeleka kwa mkopo Ziyech dakika za mwisho kabla ya Dirisha Dogo la Usajili halijafungwa usiku wa kuamkia leo, lakini PSG walisisitiza nyaraka maaluum za uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29.

Usajili wa Ziyech ulikuwa na dhamira ya kuziba nafasi ya Pablo Sarabia aliyesajiliwa Wolverhampton Wanderers ya England, baada ya kupelekwa kwa mkopo Sporting CP ya Ureno msimu wa 2021/22.

Ziyech aliyewahi kuitumikia ajax Amsterdam kabla ya kusajiliwa Chelsea mwaka 2020, amekua na wakati mgumu wa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha The Blues, akicheza michezo 56 na kufunga mabao 6.

Chelsea yavunja rekodi ya Manchester City
Robertinho aiwahi Singida Big Stars