Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru ya Serikali Jamhuri ya Watu wa China kwa kusaidia sekta ya afya ikiwemo vifaa tiba, miundombinu ya afya, dawa, mafunzo katika sekta ya afya kwa nyanja mbalimbali na timu ya madaktari wanaokuja kutoa huduma za tiba Zanzibar.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Mei 16, 2023, katika hafla ya utiaji wa saini wa ushirikiano wa miradi mitano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Zanzibar iliyofanyika Ikulu Zanzibar, ambapo pia China imesaidia Zanzibar vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 za kitanzania.

Rais Dkt. Mwinyi pia ameshuhudia utiaji saini wa mradi wa Ushirikiano wa hospitali baina ya China na Afrika, Utafiti na udhibiti wa magonjwa ya kitropiki-Kichocho, Uchunguzi wa saratani ya shingo ya Uzazi na kituo cha matibabu ya Mama na Mtoto pamoja na msaada wa vifaa tiba huku Hospitali zitakazonufaika na ushirikiano huo ni ya Mnazi Mmoja, Kivunge ,Chake chake na Abdallah Mzee.

Naye, Rais wa Chinese-African People’s Friendship Association – CAPFA, Mme Li Bin amesema urafiki uliopo wa kihistoria kati ya China na Zanzibar pamoja na ujio wa ugeni kutoka China ni kuendelea kuboresha fursa katika utalii , kutatua maradhi sugu kwa wakina Mama na fursa za miradi mbalimbali Zanzibar kwa kunufaisha pande zote za ushirikiano wa Nchi hizi na kuboresha huduma sekta ya Afya.

Mbivu na mbichi kujulikana Etihad Stadium
Young Africans kuandika historia Afrika