Serikali za China na Urusi zimetema rasmi matumizi ya fedha ya Marekani dola katika shughuli za miamala ya kibiashara kwenye nchi zao.
Taarifa ya awali imetolewa na Rais Xi Jinping wa china ambaye ametangaza habari ya kutiwa saini mapatano ya kufutwa kwa sarafu ya dola ya Marekani katika miamala ya kibiashara ya nchi yake na Urusi.
Kwa mujibu wa mapatano ya nchi hizo, dola itafutwa kabisa katika mabadilishano ya kibiashara kati yao na badala yake sarafu za mataifa hayo zitachukua nafasi ya dola katika mabadilishano.
Sambamba na matamshi hayo ya Xi Jinping serikali ya Urusi kupitia tovuti rasmi ya serikali ya Moscow, imetoa amri ya kuanza kutekelezwa kwa mapatano hayo ya mabadilishano ya kibiashara kwa kutumika sarafu za nchi hiyo(Ruble) na (Yuan).
Hayo yamejiri baada ya Rais Xi Jinping kutembelea nchi ya Urusi katika mji wa Moscow.
Ikumbukwe kuwa mwezi mei mwaka huu kampuni kubwa ya Teknolojia duniani (Google) ilitangaza kuacha kufanya kazi na kampuni ya simu iliyopo nchini China, Huawei kufuatia amri ya Marekani ya kuzuia matunizi ya vifaa vya Huawei kwa madai kuwa vinahatarisha usalama.