Kijana Tumaini Saimon Mkono aliyechukuliwa bidhaa zake aina ya ndizi barararani na mgambo wa jiji Leo amealikwa nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Robert Gabriel kwa jailli ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Mkono ambaye ni mmachinga wa matunda jijini Mwanza, ameambatana na Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula katika chakula hicho cha mchana.

Siku ya jana Jumamosi ilisambaa video iliyoonesha Mgambo wa Jiji wakimnyang’anya ndizi Mkono ambae alikua akisukuma mkokoteni katika kujitafutia riziki.

Muda mfupi baada ya Kipande hicho cha video kusambaa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa alitoa maagizo kwa Uongozi wa Mkoa wa Mwanza kuchukua hatua stahiki na kuhakikisha wanajitathmini juu ya utendaji wao.

Waziri huyo wa Tamisemi alitoa maagizo kupitia akaunti yake ya rasmi ya mtandao wa Instagram akisema, “Nimeona video inayosambaa mtandaoni ikionyesha matunda aina ya ndizi ya mfanyabiashara mdogo yakipakiwa na mgambo kwenye gari aina ya Toyota Hilux. Inasemekana tukio hili limetokea jijini Mwanza. Nimemuagiza Mkuu wa Mkoa, Robert Gabrieli kufuatilia kubainisha wahusika na hatua kali zichukuliwe dhidi yao,”

“Ninaendelea kuwaelekeza wakuu wa mikoa kote nchini kuhakikisha zoezi la kuwapanga wafanyabiashara wadogo wamachinga linafanyika kwa utulivu na amani na kujali utu. Wakurugenzi na wakuu wa wilaya mpaka haya yanatokea kwenye maeneo yenu mjitathmini kama mnatosha,” aliandika Bashungwa.

Muda mfupi baada ya Waziri huyo kutoa maagizo, RC Robert Gabriel, alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana (DC), Amina Makilagi kuwachukulia hatua mgambo saba waliodaiwa kuhusika na tukio hilo pamoja na kumsimamisha kazi mratibu wa Jiji la Mwanza wa upangaji wa wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Namuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuwaondolea hadhi ya kuwa askari wa jeshi la akiba kikosi chote kilichohusika katika tukio hilo mara moja kuanzia muda huu ikiwa na maana kwamba hawataweza kufanya kazi tena kama jeshi la akiba,” alisema.

RC Luhumbi aliongeza “Pili namsimamisha majukumu yake mratibu wa Jiji la Mwanza wa zoezi la upangaji wa machinga kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.”

Pia, Mkuu huyo wa Mkoa alilaani vikali kitendo hicho cha mgambo kuwasumbua wafanyabiashara hao.

Hii Leo baada ya hatua hizo kuchukuliwa, Waziri Bashungwa aliandika tena katika ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram akipongeza hatua zote zilizochukuliwa na kuonesha kwa hisia namna alivyochukizwa na kitendo hicho.

“Nampongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel, kwa kuchukua hatua ndani ya masaa 24 niliyomuagiza, kitendo hicho cha kikatili na cha kukosa utu kilinikwaza sana ningekua Mwanza mtu angekula Hedi,”

Aliongeza, Wake wa Mike endeleeni na zoezi la lutenga maeneo rafiki kwa biashara ya Machinga, kuyawekea miundombinu rafiki, kuwapanga kwenye maeneo kwa utaratibu, unaoheshimu utu, kuwapa elimu ya biashara na kuwaunganisha na bima na taasisi za bedha na kuepuka kuendesha operesheni za uharibifu wa mali.” Aliandika Bashungwa.

Jiji la Mwanza ni moja ya majiji ambayo yamekua na migogoro ya mara kwa mara inayohusisha wafanyabiashara ndogondogo na Mgambo wa Jiji ambao wanasimamiwa na Halmashauri ya Jiji.

Aliyefuga nyoka 124 nyumbani kwake auawa na nyoka
Waumini wamzuia Mchungaji kuendesha Ibada ya Pasaka