Chris Brown na Lil Baby wanatarajia kufanya ziara ya pamoja ya mfululizo wa maonyesho kadhaa katika msimu huu wa joto huko nchini Marekani, wakianza na shoo kubwa huko Raleigh.

Ziara hiyo iliyopewa jina la ‘The One of Them Ones’, inatarajiwa kuanza mapema Julai 15 na kuendelea hadi Agosti 27 ambapo itazunguka katika maeneno mbali mbali ikiwamo New York City, Toronto, Chicago, Atlanta, Los Angeles, Las Vegas, na maeneo mengine kadhaa.

Taarifa za ziara hiyo zimekuja siku chache baada ya kutolewa kwa video rasmi ya Ed Sheeran ‘2step’ remix akimshirikisha Lil Baby , ambaye pia mwezi huu alishiriki jozi ya video mpya za solo ikiwa ni pamoja na kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella kama sehemu ya kujirejesha vyema kwenye sanaa.

Nje ya ujio wa ziara hiyo, kwa upande wa Chris Brown, wiki hii yeye alitangazwa kushirikiana na Renowned’s John Dean kwenye mradi wa NFT unaoitwa The Auracles.

Pia mwezi huu, Brown alishiriki wimbo wake mpya uitwao “WE (Warm Embrace),” uliotayarishwa na Don City. Wimbo uliotanguliwa na ‘Iffy’ alioutoa mapema Januari 2022.

Chris brown na Lil baby si washindani kimuziki, lakini kuna funzo kubwa kwenye ushirikiano baina yao, hasa kwenye kutengeneza pesa kupitia talanta zao, kibongo bongo ni mara chache kusikia aina ya ziara za namna hii.

Zenye kuwahusisha wasanii wanye kufanya vizuri kwa pamoja, jambo ambalo pengine likitazamwa linaweza kuleta muamko mkubwa kutokana na nguvu kutoka pande mbili za wasanii kukutana pamoja, umewahi kufikiri nini kitatokea mathalani msanii Ali Kiba atatangaza ziara ya pamoja na Hamornize?, Jux na Ben Paul je?

Pombe yaleta mauaji, Baba afanya mapenzi na mke wa mwanae
Sakho: Muda wa kulipa kisasi umewadia